Enock Maregesi photo

Enock Maregesi

Enock Maregesi was born in Tanzania. He is the author of KOLONIA SANTITA, a novel. In 2015 he won the Mabati-Cornell Kiswahili Prize For African Literature for KOLONIA SANTITA. The prize has the express goal in recognizing excellent writing in African languages and encourages translation from, between and into African languages! He lives in Tanzania.

Enock Maregesi alizaliwa nchini Tanzania. Amesomea teknolojia ya habari na utawala wa biashara katika Chuo Kikuu cha Wales, na uandishi wa habari na vitabu katika chuo cha ubunifu wa kifasihi cha Manchester (The Writers Bureau) nchini Uingereza. Hadithi ya KOLONIA SANTITA: LAANA YA PANTHERA TIGRISI ni kitabu chake cha kwanza kilichohamasishwa na wakongwe wa riwaya wa Tanzania - kama Elvis Musiba, Euphrase Kezilahabi na Ben Mtobwa - na utafiti yakinifu wa miaka kumi na nane wa ujasusi, madawa ya kulevya, ugaidi wa kimataifa na silaha za maangamizi za kikemia na kibiolojia. Alizaliwa huko Mwanza mwaka 1972 na kukulia Musoma na Dar es Salaam ambako anaishi mpaka leo, akijishughulisha na biashara na uandishi wa vitabu.


“Kolonia Santita ni tofauti na hadithi zingine kwa sababu ya wapelelezi wake. Wapelelezi wake ni makomandoo-wapelelezi-wanajeshi.”
Enock Maregesi
Read more
“Nimebadili utaratibu wangu siku hizi kutokana na maadili ya watoto wetu. Siongei na watoto wangu kuhusu Mungu. Naongea na Mungu kuhusu watoto wangu. Yesu alilipa gharama ya maisha yake kutununua kutoka kwa Shetani. Tumrudie; hususan katika kipindi hiki ambacho dunia imekata tamaa.”
Enock Maregesi
Read more
“Wazazi wetu ni watu wa kuheshimu kuliko kitu chochote. Wanaweza kuona tusipoweza kuona – nyuma na mbele ya tarehe zetu za kuzaliwa.”
Enock Maregesi
Read more
“Ukitaka kuleta mabadiliko katika dunia huna budi kubadilika wewe kwanza. Ukibadilika ukawa mwema katika jamii yako umeleta mabadiliko katika dunia.”
Enock Maregesi
Read more