“Hekima ni ufunguo wa kufanya maamuzi mema kulingana na msingi wa maarifa ya Biblia.”
“Msichana wa miaka 18 miaka ya 70 ni sawa na msichana wa miaka 8 leo. Msichana wa miaka 8 leo anayajua maisha kuliko msichana wa miaka 18 miaka ya 70. Tuwape watoto wetu haki yao ya msingi ya kuwa watoto katika siku za ujana wao, kabla hawajawa watoto tena watakapokuwa wakubwa.”
“Mojawapo ya misingi ya ujasusi ni kuwa na uwezo wa kutofautisha kati ya unachojua, usichojua na unachofikiria. Unaweza kusema unajua wakati hujui. Maamuzi yasiyo sahihi ya kijasusi huweza kuiletea tume madhara makubwa.”
“Zawadi bora ya maisha kwa mwanadamu si fursa ya kufanya kazi kwa bidii na kuwa kitu fulani katika jamii. Ni amani ya Mungu katika moyo wa mwanadamu.”
“Rais wa Tume ya Dunia hakuchaguliwa kuwa kitu katika tume. Alichaguliwa kufanya kitu katika dunia.”
“Watu wanaohatarisha maisha yao kwa kudharau sheria wakati mwingine hawatakiwi kudharauliwa. Ni sawa na mtu aliyepoteza kila kitu katika maisha yake. Wana uwezo wa kufanya chochote.”