“Kuwa tajiri si kazi rahisi. Ukipata milioni ya kwanza utataka nyingine kulinda hiyo ya kwanza. Ukipata ya pili utataka mbili zingine kulinda hizo mbili za kwanza, n.k. Si kazi rahisi. Si kama unavyofikiria. Utajiri haujanipa furaha. Umenipa uhuru. Ndugu zangu ni maskini wa kutupwa. Ningependa kuishi kama maskini mwenye pesa nyingi.”
“Usalama wa Taifa ni akili si ukali. Kazi yake, au wajibu wake; ni kukusanya, kuchanganua, kudurusu na kuunganisha kwa makini, taarifa nyeti za kijasusi za ndani na nje ya nchi kuilinda Tanzania na watu wake. Ukitaka kuwa na akili kuwa kawaida. Ukitaka kuwa na nguvu kuwa mkarimu. Ukitaka kuwa tajiri kuwa tajiri wa unyenyekevu.”
“Heri kufuta mashtaka kuliko kumfunga mtuhumiwa asiyekuwa na makosa. Kuonewa kunauma.”
“Heri kuogopwa kuliko kupendwa kama huwezi kuogopwa na kupendwa kwa wakati mmoja.”
“Kufanikiwa katika maisha ni kuwa tayari muda wowote kujitoa mhanga kwa ajili ya kitu unachoweza kuwa.”