“Iwapo kila mtu atamheshimu mwenzake kama anavyojiheshimu mwenyewe; tunaweza kuishi mbinguni duniani ... lakini kwanza tuwe na maarifa binafsi.”
“Kila mtu hapa duniani ni jirani yako. Hakuna mtu mwingine hapa ulimwenguni isipokuwa sisi. Lazima tujifunze kuishi pamoja.”
“Kuwa tajiri si kazi rahisi. Ukipata milioni ya kwanza utataka nyingine kulinda hiyo ya kwanza. Ukipata ya pili utataka mbili zingine kulinda hizo mbili za kwanza, n.k. Si kazi rahisi. Si kama unavyofikiria. Utajiri haujanipa furaha. Umenipa uhuru. Ndugu zangu ni maskini wa kutupwa. Ningependa kuishi kama maskini mwenye pesa nyingi.”
“Watu wanaohatarisha maisha yao kwa kudharau sheria wakati mwingine hawatakiwi kudharauliwa. Ni sawa na mtu aliyepoteza kila kitu katika maisha yake. Wana uwezo wa kufanya chochote.”
“Kitu cha kwanza kufanya kama umeamua kuficha ukweli wape watu ukweli mwingine.”
“Serikali haifungi mtu kutokana na shinikizo la watu. Inafunga mtu kutokana na sheria za nchi.”
“Usitegemee malaika ashuke kutoka mbinguni kuja kukutatulia shida zilizokushinda kwa uzembe. Malaika ni wewe mwenyewe. Ukifanya unachoweza kufanya, Mungu atafanya usichoweza kufanya.”