“Joram Kiango ni mpelelezi maarufu nchini Tanzania. Willy Gamba ni mpelelezi maarufu katika bara la Afrika. John Murphy ni mpelelezi maarufu duniani. Ni watu watatu tofauti wanaofanya kazi zinazofanana.”
“Watu wa kulisaidia bara la Afrika hawatatoka Amerika au kwingineko. Afrika ni tatizo letu. Watatoka Afrika kwenyewe.”
“Kolonia Santita ni tofauti na hadithi zingine kwa sababu ya wapelelezi wake. Wapelelezi wake ni makomandoo-wapelelezi-wanajeshi.”
“Usalama wa Taifa ni akili si ukali. Kazi yake, au wajibu wake; ni kukusanya, kuchanganua, kudurusu na kuunganisha kwa makini, taarifa nyeti za kijasusi za ndani na nje ya nchi kuilinda Tanzania na watu wake. Ukitaka kuwa na akili kuwa kawaida. Ukitaka kuwa na nguvu kuwa mkarimu. Ukitaka kuwa tajiri kuwa tajiri wa unyenyekevu.”
“Zawadi bora ya maisha kwa mwanadamu si fursa ya kufanya kazi kwa bidii na kuwa kitu fulani katika jamii. Ni amani ya Mungu katika moyo wa mwanadamu.”
“Kujiua ni ubinafsi kwa sababu ya watu wanaokupenda.”
“Kujiingiza katika madawa ni matokeo ya maisha. Hatutumii madawa ya kulevya. Madawa ya kulevya ni sisi wenyewe; tunahitaji kusaidiwa.”