“Kuwa tajiri si kazi rahisi. Ukipata milioni ya kwanza utataka nyingine kulinda hiyo ya kwanza. Ukipata ya pili utataka mbili zingine kulinda hizo mbili za kwanza, n.k. Si kazi rahisi. Si kama unavyofikiria. Utajiri haujanipa furaha. Umenipa uhuru. Ndugu zangu ni maskini wa kutupwa. Ningependa kuishi kama maskini mwenye pesa nyingi.”
“Heri kuwa maskini mwenye pesa nyingi kuliko tajiri mwenye mifuko iliyotoboka.”
“Usalama wa Taifa ni akili si ukali. Kazi yake, au wajibu wake; ni kukusanya, kuchanganua, kudurusu na kuunganisha kwa makini, taarifa nyeti za kijasusi za ndani na nje ya nchi kuilinda Tanzania na watu wake. Ukitaka kuwa na akili kuwa kawaida. Ukitaka kuwa na nguvu kuwa mkarimu. Ukitaka kuwa tajiri kuwa tajiri wa unyenyekevu.”
“Zawadi bora ya maisha kwa mwanadamu si fursa ya kufanya kazi kwa bidii na kuwa kitu fulani katika jamii. Ni amani ya Mungu katika moyo wa mwanadamu.”
“Iwapo kila mtu atamheshimu mwenzake kama anavyojiheshimu mwenyewe; tunaweza kuishi mbinguni duniani ... lakini kwanza tuwe na maarifa binafsi.”
“Kitu cha kwanza kufanya kama umeamua kuficha ukweli wape watu ukweli mwingine.”
“Vichwa vitatu vya sururu na chembe tatu za bunduki za Kalashnikov; na alama ya bahati, mafanikio, udhalimu na mwanzo mpya ya msalaba wa swastika, kama alama ya ujenzi na uhalifu wa Kolonia Santita.”