“Nimebadili utaratibu wangu siku hizi kutokana na maadili ya watoto wetu. Siongei na watoto wangu kuhusu Mungu. Naongea na Mungu kuhusu watoto wangu. Yesu alilipa gharama ya maisha yake kutununua kutoka kwa Shetani. Tumrudie; hususan katika kipindi hiki ambacho dunia imekata tamaa.”
“Nafasi yako peponi itapotea iwapo utamruhusu Pluto (kiongozi wa ahera) akukaribishe bazarai (makao makuu ya ahera) kwa kuchukua maisha yako mwenyewe. Kujiua ni kujipenda zaidi kuliko unaowapenda. Anayejiua hujifikiria zaidi yeye kuliko wengine.”
“Mihadarati ni chanzo kikubwa cha matatizo ya wanadamu. Mshahara wake ni wazimu, uhalifu na mauti.”
“Sema hapana kwa ndiyo nyingi kwa sababu hawaoni unachokiona. Ndoto yako waijua mwenyewe.”
“Watu hawaheshimu wewe ni nani au unatoka wapi. Wanaheshimu nguvu ya matendo yako.”
“Kila mtu hapa duniani ni jirani yako. Hakuna mtu mwingine hapa ulimwenguni isipokuwa sisi. Lazima tujifunze kuishi pamoja.”