“Sema hapana kwa ndiyo nyingi kwa sababu hawaoni unachokiona. Ndoto yako waijua mwenyewe.”
“Kujiua ni ubinafsi kwa sababu ya watu wanaokupenda.”
“Nafasi yako peponi itapotea iwapo utamruhusu Pluto (kiongozi wa ahera) akukaribishe bazarai (makao makuu ya ahera) kwa kuchukua maisha yako mwenyewe. Kujiua ni kujipenda zaidi kuliko unaowapenda. Anayejiua hujifikiria zaidi yeye kuliko wengine.”
“Kolonia Santita ni tofauti na hadithi zingine kwa sababu ya wapelelezi wake. Wapelelezi wake ni makomandoo-wapelelezi-wanajeshi.”
“Migogoro inatokea kwa sababu watu wameshindwa kuheshimiana. Ukijiheshimu na ukaheshimu wengine; utaacha dunia katika hali nzuri kuliko ulivyoikuta, wakati ukiingia.”
“Usitegemee malaika ashuke kutoka mbinguni kuja kukutatulia shida zilizokushinda kwa uzembe. Malaika ni wewe mwenyewe. Ukifanya unachoweza kufanya, Mungu atafanya usichoweza kufanya.”