“Usitegemee malaika ashuke kutoka mbinguni kuja kukutatulia shida zilizokushinda kwa uzembe. Malaika ni wewe mwenyewe. Ukifanya unachoweza kufanya, Mungu atafanya usichoweza kufanya.”

Enock Maregesi

Explore This Quote Further

Quote by Enock Maregesi: “Usitegemee malaika ashuke kutoka mbinguni kuja k… - Image 1

Similar quotes

“Kufanya kosa huku ukijua ni kosa ni kujiombea jela mwenyewe.”


“Zawadi bora ya maisha kwa mwanadamu si fursa ya kufanya kazi kwa bidii na kuwa kitu fulani katika jamii. Ni amani ya Mungu katika moyo wa mwanadamu.”


“Watu wanaohatarisha maisha yao kwa kudharau sheria wakati mwingine hawatakiwi kudharauliwa. Ni sawa na mtu aliyepoteza kila kitu katika maisha yake. Wana uwezo wa kufanya chochote.”


“Hekima ni ufunguo wa kufanya maamuzi mema kulingana na msingi wa maarifa ya Biblia.”


“Kufanikiwa katika maisha ni kuwa tayari muda wowote kujitoa mhanga kwa ajili ya kitu unachoweza kuwa.”


“Nimebadili utaratibu wangu siku hizi kutokana na maadili ya watoto wetu. Siongei na watoto wangu kuhusu Mungu. Naongea na Mungu kuhusu watoto wangu. Yesu alilipa gharama ya maisha yake kutununua kutoka kwa Shetani. Tumrudie; hususan katika kipindi hiki ambacho dunia imekata tamaa.”